Job Details
- Location: Dar es Salaam, Manyara
Job Description
🔨 Auction
🚗 Vehicles & Motorcycles
Public auction
⏰ In 8 days
🏢 So They Can Tanzania
📅 Auction date and time
Monday, 16 November 2026 · 10:00 AM
📍 Venue
Ofisi ya So They Can Tanzania, Na.1, Mtaa wa Sinza, Nyunguu, Babati, Manyara
👁 Inspection
Saa 03:00 asubuhi – saa 11:00 jioni
💰 Deposit / payment
100%
📅 Add to Google Calendar
Share on WhatsApp
🗺 Map
Original notice and documents →
Wito wa zabuni: Uuzaji wa trekta
ZABUNI NAMBA: STC/TZ/ADV/2026/02
Shirika la So They Can Tanzania linategemea kuuza trekta, mali ya shirika. Mauzo ya trekta hilo yanazingatia mahali trekta lilipo na hali yake ya sasa “Kama Lilivyo, Mahali Lilipo”
Maelezo ya trekta
Aina ya trekta: John Deere
Namba ya Usajili: T 958 CDY
Mwaka wa Kutengenezwa: 2012
Modeli: 5503
Chesesi Namba: PY5503E003356
Hali ya Injini: Nzuri
Aina ya Mafuta: Dizeli
Mfumo wa Giabox: Manual
Rangi ya Nje: Kijani
Hali ya Tairi: Nzuri
Bima: Inaisha 18 Desemba 2026
Masharti na vigezo vya uuzaji
- Kama Lilivyo, Mahali Lilipo
Trekta litauzwa kulingana na hali yake ya sasa. Waombaji wanashauriwa kulikagua kabla ya kuwasilisha maombi yao ya manunuzi.
- Uwasilishaji wa maombi ya manunuzi
Maombi lazima yawasilishwe katika ofisi za So They Can Tanzania, Nyumba namba 1, Mtaa wa Sinza, Nyunguu, Babati, kwenye bahasha iliyofungwa ikiwa imeandikwa “Maombi ya ununuzi wa trekta – T 958 CDY” au maombi yatumwe kwa barua pepe kwenda
[email protected]
.
Mwisho wa kutuma maombi hayo ni Jumatatu tarehe 16 November 2026 saa 11:00 jioni.
- Masharti ya malipo
Mwombaji atakayepitishwa kununua trekta husika atatakiwa kufanya malipo kwa asilimia 100% ya bei ya manunuzi, kupitia akaunti ya benki ya So They Can Tanzania ndani ya siku saba baada ya kupokea taarifa ya kukubaliwa ombi la manunuzi, Taarifa hii itatolewa tarehe 21 Novemba 2026
- Kodi, ada za kisheria, na gharama za uhamisho
Mnunuzi atatakiwa kulipia gharama zote zinazohusiana na uhamisho wa umiliki wa trekta, kodi husika, ada za uhamisho, na gharama ya kadi mpya ya usajili.
- Uchukuaji wa trekta
Mnunuzi atatakiwa kuichukua trekta ndani ya siku tano (5) baada ya kukamilisha malipo, na uhamisho wa umiliki, na kufikisha nakala ya kadi ya umiliki mpya kwenye ofisi za So They Can Tanzania.
Sera ya kutokuvumilia rushwa, ufisadi, na ughushi
So They Can Tanzania inaendeshwa chini ya sera ya kutokuvumilia kabisa (zero-tolerance) kuhusiana na rushwa, ufisadi, ughushi, njama za siri. Jaribio lolote kutoka kwa mwombaji, wakala wao, au mwakilishi, kutoa ahadi, au kutoa zawadi yoyote, rushwa, kamisheni, au kivutio cha kifedha kwa mfanyakazi au mwakilishi yeyote wa So They Can Tanzania kitasababisha kuondolewa mara moja kwa zabuni hiyo.
Njama kati ya waombaji ili kupanga bei au kuchezea matokeo ya mchakato huu wa zabuni zimepigwa marufuku vikali na zitasababisha kukataliwa kwa moja kwa moja na uwezekano wa kuripotiwa kisheria. Shaka au ushahidi wowote wa shughuli za ughushi, maelezo ya uongo, au vitendo vya kifisadi vitasababisha kusitishwa mara moja kwa mkataba wa uuzaji.
Ufichuaji / Uripoti wa Siri
Waombaji wanaoshuhudia au kushuku tabia yoyote ya kifisadi au ya ughushi inayohusiana na zabuni hii wanaweza kuripoti kwa siri kupitia
Ukaguzi na maswali
Ukaguzi wa trekta
Mwombaji anaweza kuomba kukagua trekta kupitia namba za mawasiliano hapo chini.
Tarehe za kukagua: 9 hadi 13 November 2026
Muda: Saa 03:00 asubuhi – saa 11:00 jioni
Eneo: Ofisi ya So They Can Tanzania, Na.1, Mtaa wa Sinza, Nyunguu, Babati, Manyara
Namba za mawasiliano So They Can Tanzania
John Jonas Mwakipesile, Afisa Mawasiliano
Simu: +255 687 128 570
Noel Patrick Mndalila, Dereva
Simu: +255 753 937 175
Barua Pepe Rasmi
Tamko la uaminifu la mwombaji
Wakati wa uwasilishaji wa maombi ya ununuzi wa trekta, waombaji wanatakiwa kusaini kauli hii fupi pamoja na maombi yao:
“Mimi/Sisi tunathibitisha kuwa nimesoma/tumesoma, nimeelewa/tumeelewa, na ninakubali/tunakubali kuzingatia Sera ya So They Can Tanzania Dhidi ya Rushwa, Ufisadi, na Ughushi. Mimi/Sisi tunathibitisha kuwa maombi haya yamefanywa bila makubaliano yoyote ya awali, njama, au mipango na mwombaji mwingine yeyote au mfanyakazi yeyote wa So They Can Tanzania.”
Sahihi: ___________________________
Jina: ______________________________
Tarehe: ____________________________
Explore more
Explore More Jobs
Browse other opportunities in these areas.
Browse by Location
View all locations
→
More Jobs in Dar es Salaam
More Jobs in Manyara
Browse by Category
View all categories
More Jobs: Administration Jobs
How to Apply
Application link: Apply for this job
0 Response to Auction: Zabuni Ya Ununuzi Wa Trekta Aina Ya John Deere 5503